Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ambaye ni raia wa Ufaransa amefunguka juu ya mwenendo wa klabu yake na nini anakiona kwa klabu hiyo mara baada ya kutopata ushindi katika michezo mitatu mfululizo na huku akitoka kutoka sare jana usiku dhidi ya West Ham kwa sare ya 0-0.
Wenger alipohojiwa alisema "sisi kama timu tunatakiwa kupambana na kupambana zaidi maana bado hatujakata tamaa kuhusu kuwania taji la ligi kuu"
"ni kweli tumeachwa mbali na Manchester city, lakini kuna tofauti ya kuachwa mbali na kukata tamaa, bado hatujakata tamaa ila tunaendelea kupambana kushinda ligi kuu" alisema Wenger ambaye kwa sasa klabu yake inashika nafasi ya 7 katika msimamo wa ligi kuu, huku akiwa kazidiwa alama 19 na Manchester city iliyoko kileleni.
"ligi bado haijaisha, kwa hiyo bado sijaamini kama Manchester city wanastahili kuitwa mabingwa" alimalizia mzee Arsene Wenger.
Kwa kauli hiyo, Wenger anakuwa tofauti na kocha wa Chelsea, Antonio Conte ambaye mara baada ya kipigo kutoka kwa West Ham cha 1-0 jumamosi iliyopita, kocha huyo muitaliano alisema "sidhani kama Chelsea ipo ili kushindania taji, haipo sawa na sizani kama itakuwa sawa kuwania taji kushindana na klabu kama Man city ambayo haijapoteza mchezo wowote wakati Chelsea katika michezo 16 ishapoteza michezo 4"
Sasa wakati Conte akiiongoza Chelsea ikishika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu na kocha wake anasema haioni Chelsea ikipambania ubingwa lakini Arsene Wenger aliye nafasi ya saba na Arsenal yake anasema bado anaweza kutwaa taji la ligi kuu!
Toa maoni yako hapo chini?
Post a Comment
Post a Comment