Mara baada ya Kenya kufanikiwa kufudhu kucheza fainali ya kombe la Cecafa Chalenji hapo jana mara baada ya kuifunga Burundi 1-0 sasa leo ni zamu ya Zanzibar ikishuka kumenyana na Uganda katika nusu fainali ya pili.
Zanzibar leo itashuka uwanjani kumenyana na Uganda ambapo kihistoria timu ya Uganda ambao ni mabingwa watetezi wa kombe hilo wanabebwa vyema na historia katika michezo waliyokutana timu hizo mbili.
Katika michezo minne iliyopita, Uganda ameshinda michezo mitatu na kupoteza mmoja kwa matuta walipomenyana na Zanzibar huko nyuma.
Mchezo huo utachezwa jioni ya leo mnamo saa 15:00 huko nchini Kenya ambapo inafanyika michuano hiyo.
Post a Comment
Post a Comment