Real Madrid inashuka dimbani leo katika mchezo wa Klabu bingwa ya Dunia ambapo Madrid inashiriki kama bingwa wa Ulaya lakini pia akiwa kama bingwa mtetezi wa taji hilo aliloshinda mwaka jana.
Real Madrid itashuka katika mchezo huu muhimu kumenyana na wababe wa bara la Asia, Al Jazira ambapo kuelekea katika mchezo huo, kocha wa klabu hiyo ametania kuwa ili kuwazuia Madrid leo basi itamlazimu amuombe basi (mfumo wa kukaba zaidi) kocha wa Manchester united, Jose Mourinho ambaye amekuwa akisifika kwa kukaba zaidi kuliko kushambulia.
Mchezo huo utachezwa saa 20:00 huko katika nchi za kiarabu.
(picha ya chini ni kikosi kamili cha Real Madrid katika mchezo huu)
Post a Comment
Post a Comment