Nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amewafumba mdomo wale wote wanaombeza juu ya tunzo yake aliyobeba wiki kadhaa zilizopita kama mchezaji bora wa mwaka mara baada ya leo kudhihirisha tena kuwa yeye sio mtu wa mchezo mara baada ya kuisaidia klabu yake kufudhu kucheza fainali ya klabu bingwa ya dunia (CWC) katika mchezo walioshinda 2-1 dhidi ya Al Jazira uko Abu Dhabi.

Al Jazira ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 41 kupitia kwa Romarinho, raia wa Brazil na kufanya mchezo kwenda mapumziko huku Madrid wakiwa nyuma.

Kipindi cha pili kilianza na Real Madrid wakachomoa kupitia kwa nyota wake Ronaldo akifunga goli lililomfanya kuwa mfungaji bora wa muda wote katika michuano hiyo akiwa na magoli 6 na kufanya matokeo kuwa 1-1 kabla ya Gareth Bale kufunga goli la pili katika dakika za majeruhi na kuufanya mchezo kuisha kwa Madrid kushinda 2-1 huku Real Madrid ikifanikiwa kufudhu kucheza fainali.

Ingawa pia mchezo huo umekuwa na matukio ya kukataliwa magoli matatu kutokana na teknolojia ya refa wa video (VAR), Real Madrid wakikataliwa magoli mawili na Al Jazira goli moja.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.