Nchini Uingereza kwa sasa ni kila mtu anaiongelea Manchester city na moto iliyokuwa nayo mara baada ya kuweka rekodi mpya katika ligi kuu Uingereza kwa sasa ikiwa ni klabu iliyoshinda michezo mingi mfululizo kwa michezo 15, ikiivunja rekodi iliyokuwa imewekwa na Arsenal ya michezo 14 mara baada ya usiku wa leo kushinda mchezo muhimu dhidi ya Swansea, ugenini Liberty Stadium.

Manchester city imeweka rekodi hiyo ikishinda 4-0, huku magoli yao yakifungwa na David Silva aliyefunga mara mbili (akifunga pia mara nne katika michezo mitatu ya ligi kuu), Kevin De Bruyne pamoja na Kun Aguero.

Kwa ushindi huo pia unaifanya Manchester city kushinda michezo 16 kati ya 17 huku ikitoa suluhu mmoja na kufikisha alama 49 na kuiacha Chelsea inayoshika nafasi ya tatu kwa alama 14 huku Manchester city ikishika nafasi ya pili ikiwa na alama 38 mara baada ya usiku wa leo kupata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Bournemouth, goli likifungwa na Romelu Lukaku.

Matokeo mengine EPL;
West Ham 0-0 Arsenal
Tottenham 2-0 Brighton
Liverpool 0-0 West Brom
Southampton 1-4 Leicester
Newcastle 0-1 Everton

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.