Klabu ya PSG imepata ushindi muhimu katika mchezo wa kombe la ligi la Ufaransa, usiku wa leo ikiwa ugenini katika uwanja wa Stade de la Imenau dhidi ya wababe wao Strasbrough kwa kushinda magoli 2-4.
Magoli ya PSG yalianza kufungwa na Sammier, mchezaji wa Strasbrough aliyejifunga na kuifanya PSG kuwa mbele kabla ya Angel Di Maria kufunga goli jengine na kisha Dani Alves na Julia Draxler kufunga magoli mengine na kukamilisha idadi ya 4-2.
Lakini haikuwa kazi rahisi kwa PSG ikicheza na klabu hii ambayo ndiyo iliharibu rekodi ya PSG ya kushinda mfululizo msimu huu katika ligi kuu ikiwa ndio klabu ya kwanza kuifunga PSG, ikiifunga 2-1 katika mchezo wa ligi kuu wiki kadhaa zilizopita.
Kwa maana hiyo katika mchezo huu, PSG ilishuka ikiwa inajua kuwa inacheza na bingwa wake aliyepanda daraja msimu huu lakini alishamfunga wiki kadhaa nyuma.
Matokeo mengine kombe la ligi Ufaransa (French League Cup);
Montepillier 4-1 Lyon
Lille 3-4 OGC Nice
Rennes 6-5 Marseille
Post a Comment
Post a Comment