Katika mchezo muhimu wa kombe la ligi la Italia, Copa Italia, klabu ya Ac Milan iliyo chini ya kocha mbabe, Gennaro Gattuso imepata ushindi wake wa pili mfululizo mara baada ya kuitandika klabu ya Verona magoli 3-0 na kufanikiwa kufuzu kucheza hatua inayofata ambapo huko itamenyana na Inter Milan.
Magoli ya Ac Milan yakifungwa na Suso, Romagnoli na Crutone na kufanya Ac Milan kushinda 3-0. Huku Suso akiendelea kung'aa baada ya kufunga moja na kutengeneza bao jengine.
Baada ya ushindi huo, kocha huyo alisema "mashabiki na wapenzi wa Ac Milan wanatakiwa kuwa sawa na klabu na kuipatia nguvu na kuwa nayo pamoja wakati klabu ikiwa inaelekea kukutana na michezo migumu ukiwemo wa 'derby' dhidi ya Inter" alisema Gattuso ambaye ameanza kutumia mfumo wa 4-3-3 unaoipa mafanikio kwa sasa AC Milan.
Matokeo mengine Copa Italia;
Fiorentina 3-2 Sampordia
Post a Comment
Post a Comment