"Je Arsene Wenger ataendelea kubaki Arsenal?" ndilo swali alilouliza mchezaji wa zamani wa Arsenal, Martin Keown ambaye kwa sasa ni mchambua soka huko nchini Uingereza akiuliza hivyo mara baada ya klabu hiyo kutoka suluhu usiku wa kuamkia leo dhidi ya West Ham, suluhu ya 0-0 na kushuhudiwa Arsenal ikiporomoka kutoka nafasi ya 5 mpaka nafasi ya 7 katika msimamo wa ligi kuu Uingereza.
Akiwa katika uchambuzi wake, Martin Keown alisema "siioni Arsenal ikiwa katika makali yake, naiona inavurunda na kucheza ovyo kila siku. Siioni Arsenal ikipambana kuwania mataji, siioni Arsenal ikipambana dhidi klabu kubwa katika mataji. Siioni Arsenal ikifuzu kiurahisi kucheza Uefa msimu ujao" alisema Keown.
Lakini pia kwa mchambuzi mwengine, Rio Ferdinand ambaye alikuwa mchezaji wa Manchester united alisema "siioni Arsenal ya miaka ile ya Vieira, naiona Arsenal ambayo wachezaji wake hawana hali ya mchezo na ya kushinda. Wachezaji wa Arsenal baada ya kushambulia kwenda mbele wao wanarudi nyuma"
Ni baadhi ya kauli zilizotolewa na baadhi ya wachambuzi wa soka kuhusu mwenendo mbovu wa Arsenal.
Je Arsene Wenger ataendelea kubaki Arsenal mpaka msimu ujao?
Post a Comment
Post a Comment