Klabu ya Newcastle inayoshika nafasi ya 16 katika msimamo wa ligi ikiwa na alama 15 tu. Lakini ukifika mzunguko wa pili wa ligi kuu, huenda ikawa sio Newcastle ya sasa ikiwa imetoka kupoteza mchezo wake katika raundi ya 17 ikifungwa 0-1 dhidi ya Everton.
Kwanini itakuwa moto?
Kupitia kwa mmiliki wa klabu hiyo Mike Ashley ana mpango wa kutoa dau kubwa katika usajili ili kocha wa klabu hiyo Rafa Benitez aweze kufanya usajili mkubwa mwezi januari katika dirisha dogo la usajili.
Mpango wake ni nini?
Mpango wa mmiliki huyo kutoa dau la usajili ili kuinusuru klabu hiyo isiweze kushuka daraja ili aiuze klabu hiyo kwa mwanamama Amanda Staveley ambaye yeye na kampuni yake ya PCP wamefikia katika makubaliano mazuri ya kuiuza klabu hiyo ingawa kikwazo kilichopo, mama huyo anaogopa kununua klabu itakayoshuka daraja.
Kwa maana hiyo, ili Mike Ashley afanikiwe kuiuza klabu hiyo kwa Amanda, basi inabidi aiweke Newcastle iwe vizuri, ipambane ili isishuke daraja.
Dili lipoje?
Mpaka sasa mnunuzi huyo yupo kwenye hatua za mwisho kuinunua klabu hiyo ambapo yupo tayari kutoa kiasi cha paundi milioni 300 ili ainunue klabu hiyo ingawa kusuasua kwake ni kutokana na kuogopa kushuka daraja kwa Newcastle.
Post a Comment
Post a Comment