Jana Manchester united ilipata ushindi wa 1-0 dhidi ya Afc Bournemouth goli likifungwa na Romelu Lukaku, ushindi ambao umekuja baada ya kipigo kutoka kwa Manchester city jumapili iliyopita na kuifanya Manchester city kuwa mbele ya Man utd kwa alama 11 huku ikiwa kileleni na wengi wakiizungumzia Manchester city kama ndiye atakayekuwa bingwa msimu mara baada ya tena jana kuweka rekodi ya kushinda michezo 15 mfululizo kwa msimu mmoja baada ya ushindi wa goli 4-0.
Baada ya maneno ya wengi wakiitabiria ubingwa kwa Manchester city, umeyaskia maneno ya kocha Jose Mourinho?
"kivipi Manchester city awe bingwa wakati ligi imeisha? wana timu bora ila bado sio mabingwa, bingwa wa ligi ataonekana mwezi wa tano ligi ikiwa mwishoni. Kama mwezi huu tu Manchester city ashakuwa bingwa basi mi ningekuwa zangu matembezini Brazil au Los Angeles" alisema Mourinho akipinga maneno ya watu wakiipa ubingwa Manchester city.
"ni kweli walitufunga, na wana kikosi bora lakini sio kwamba tumeshakubali kuwa tumeshindwa" aliongeza Mourinho.
Post a Comment
Post a Comment