Mlinzi wa klabu ya Manchester city, Kyle Walker ambaye ni raia wa Uingereza jana alikuwa mtu mwenye furaha mara baada ya kucheza uwanja mmoja na mlinzi wa Brazil, Dani Alves.
Mara baada ya mchezo uliozikutanisha Uingereza dhidi ya Brazil ulioisha kwa suluhu ya bila kufungana yaani 0-0, walinzi hao wa kulia walikutana na kukumbatiana na Walker kutuma katika mtandao maneno yaliyosomeka "Ni furaha kucheza dhidi ya timu kubwa duniani na kucheza na mchezaji bora kama Dani Alves, amekuwa akinivutia siku zote"
Post a Comment
Post a Comment