Ni wiki mpya tumeianza, wiki ambayo Tanzania tutashuhudia michezo ya kugombani taji la Tanzania katika michuano ya Baseball itakayofanyika pale Dar es Salaam katika viwanja vya shule ya Azania Sekondari siku ya tarehe 1 mwezi desemba ambapo itakamilika tarehe 3 ya mwezi huo.
Hapa nakuletea mfululizo wa makala ambayo itahusu kukujuza tofauti ya mchezo huu wa Baseball na mchezo wa Cricket.
Kwanini nimekuletea Baseball na Cricket, kama tunavyofahamu duniani kote kuna michezo mingi zaidi ya 50, na katika michezo hiyo kuna michezo inafanana na inaweza ikakuchanganya usitambue upi ni upi, kama mpira wa kikapu (basketball) na netball, mieleka na mchezo wa masumbwi na mingine mingi.
Sasa katika michezo hiyo, kuna michezo ya Cricket na Baseball ambayo nayo inafanana kwa kiwango kikubwa.
1. Gongo la kupigia (Bat)
Tofauti ya kwanza ambayo haitokupa tabu sana kama ukiwa makini basi ni yale magongo yanayotumika kupiga mpira.
>Gongo la kupigia la mchezo wa Cricket lina umbo lenye pembe nne kali na moja imetengeneza kama bonde.
>Gongo la kupigia mpira la Baseball lina umbo la duara ambalo lenyewe linamruhusu mpiga mpira (batsman) apige mpira kuelekea eneo lake la mbele tu.

2. Mpira
Katika mpira hakuna tofauti kubwa kutokana na michezo yote kutaka mpira upigwe na uelekee katika mwelekeo fulani.
Katika mpira hakuna tofauti kubwa kutokana na michezo yote kutaka mpira upigwe na uelekee katika mwelekeo fulani.
Post a Comment
Post a Comment