Hatimaye hii ni habari nzuri kwa mashabiki wa klabu ya Manchester united mara baada ya kutoka taarifa kwa mshambuliaji wa klabu hiyo, Romelu Lukaku kunusurika na hukumu iliyokuwa inamnyemelea.
Lukaku alikuwa anazaniwa kukutwa na adhabu ya kufungiwa michezo mitatu mara baada ya kuonekana akimchezea vibaya mlinzi wa klabu ya Brighton katika mchezo wa ligi kuu zilipomenyana klabu hizo, na Man utd kuibuka na ushindi wa 1-0.
Kutokana na mchezo huo ambao aliuonyesha, chama cha soka cha nchini Uingereza, FA kilitoa taarifa ya kufanya uchunguzi wa kina wa kuchunguza video za tukio hilo na sasa imekuja na hukumu na kumuona mchezaji huyo hana hatia.
Kama angekutwa na hatia basi Lukaku angeikosa michezo mitatu ambayo ni dhidi ya Watford, Arsenal na Manchester city.
Post a Comment
Post a Comment