Nyota wa Chelsea na timu ya taifa ya Brazil, Willian Borges ametoa sifa juu ya nyota wa Chelsea anayeichezea kwa mkopo klabu ya Crystal Palace, Ruben Loftus-cheek.
Willian alitoa sifa hizo mara baada ya mchezo baina yao, Brazil dhidi ya Uingereza ambayo ndiyo timu ya Loftus-cheek na kusema "ni mchezaji mzuri, na nashangazwa kwanini aliondoka Chelsea, inabidi afanye mpango arudi" alisema Willian ambapo mchezo huo uliisha sare ya kutokufungana huku Loftus-cheek akitoka mapema kutokana na majeruhi ya mgongo.
Kuhusu kuitumia timu yake ya klabu dhidi ya Everton katika mchezo wa ligi kuu, majibu yatatolewa na kocha wake Roy Hodgson ambaye ameipokea Crystal ikiwa na msimu mbovu.
Post a Comment
Post a Comment