Nadhani umepata kusikia kuhusu yule mzee aliyepata umaarufu mara baada ya kuhudhuria katika mnada wa nyumba za Lugumi na kukatokea utata juu ya mzee huyo anayeitwa Dr. Luis Shika kwamba ye ni shabiki wa Chelsea ya nchini Uingereza.

Dr. Luis kupitia chombo kimoja cha habari alifanya nacho maongezi na alipoulizwa kuhusu soka alisema ye ni mpenzi sana wa soka la Ulaya haswa la nchini Uingereza.

"Mi nafatilia sana soka la Uingereza, nashabikia klabu ya Chelsea" alisema mzee huyo aliyebatizwa jina na kuitwa jina la Tajiri Mtata.

"naipenda Chelsea kwa vile inamilikiwa na rafiki yangu" alisema mzee Shika ambapo pia alidai tajiri na mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich ni rafiki yake na alikutana nae pindi alipoenda Urusi kusoma, nchi ambayo ndio uraia wa Roman Abramovich.

(hapo kwenye picha Dr. Luis akiwa na mchambuzi wa michezo, Saleh Juma.)

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.