Klabu ya Everton ya nchini imepigwa chini juu katika usajili wanaotaka kuufanya kwa klabu ya Watford ambapo zote zinashiriki ligi kuu Uingereza.
Klabu ya Everton ilipeleka maombi ya kutaka kumsajili kocha wa Watford, Marco Silva ambapo iliandaa dau la paundi milioni 8.5, dau ambalo Watford wameona halifai kwa thamani ya kocha wao.
Everton kwa sasa ipo chini ya kocha msaidizi mara baada ya kocha mkuu, Ronald Koeman kutimuliwa kutokana na kiwango kibovu alichokionyesha kwa kusababisha timu kutokufanya vizuri licha ya kutumia kiasi kikubwa kwenye usajili, akiwasajili nyota kama Glyfi Sigurdsson, Klaasen, Michael Keane na Wayne Rooney aliyemchukua bure akitokea Manchester united
Post a Comment
Post a Comment