Moja kati ya viungo bora duniani, Angel Di Maria alishawai kucheza Man utd ambapo kwa sasa anacheza pale Ufaransa kwenye klabu ya PSG.
Hakukaa muda mrefu pale klabuni Man utd ambapo alisajiliwa mwaka 2014 kwa dau la paundi milioni 54 akitokea Real Madrid na kuichezea klabu hiyo michezo 27 tu kisha mwaka 2015 kuondoka klabuni hapo na kujiunga na PSG.
Je unajua sababu ya mchezaji huyo nyota aliyetegemewa kufanya makubwa pale Manchester kuachana na klabu hiyo kwa muda mfupi?
Hii ndiyo sababu inayoelezwa na mtu wa karibu wa Angel Di Maria kwanini hakudumu klabuni Man utd kipindi icho ikiwa chini ya kocha Van Gaal.
Mtu huyo wa karibu anaeleza "sababu mbili zilizomfanya Di Maria aachane na Man utd ni kwamba, sababu ya kwanza alikuwa anapata tabu kuwasiliana na kuwa na mahusiano mazuri akiwa pale lakini pia sababu kubwa ni kwamba, viongozi wa Man utd walichokihitaji kutoka kwa Di Maria ni kuuza jezi nyingi kupitia nyota yake na ubora wake. Na sio kuipatia mafanikio klabu na mashabiki kuwapa furaha"
Di Maria katika michezo hiyo 27 alifanikiwa kufunga magoli matatu tu, lakini pia mtu huyo wa karibu wa Di Maria aliongezea "inavyoonyesha, viongozi wa Man utd toka kuondoka kwa kocha Alex Ferguson kikubwa wanachotaka kukifanya ni kutengeneza pesa zaidi kuliko hata kuangalia mashabiki watapata vipi furaha."
Klabu ya Man utd imekuwa haina mwenendo mzuri toka kuondoka kwa Ferguson ambapo yeye ndiye aliyekuwa kocha wa mwisho kumaliza katika timu 3 za juu ambapo msimu wake wa mwisho klabuni hapo aliisaidia klabu hiyo kubeba Ligi kuu Uingereza.
Post a Comment
Post a Comment