Gwiji wa soka Ronaldo De Lima ameipongeza klabu yake ya zamani ya nchini Brazil, Corithians kwa kufanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu nchini humo.
Corithians imefanikiwa kutwaa ubingwa wake wa ligi kuu nchini Brazil mara saba mara baada ya ushindi wake dhidi ya watani wao Fluminense wa mabao 3-1, magoli ya Corithians yakifungwa na mchezaji wa zamani wa Brazil na Manchester city, Jo aliyefunga mara mbili na Jadson na kuifanya klabu yao kutwaa taji hilo la ikiwa imebakiza michezo 3.
Ronaldo De Lima kupitia mtandao wa Instagram aliipongeza klabu hiyo.
Post a Comment
Post a Comment