Timu ya taifa ya Italia ina kazi ya kujitetea kushiriki kucheza kombe la dunia mwakani huko nchini Urusi.

Italia ina kazi ngumu usiku huu ikiwa inashuka uwanjani kumenyana na Sweden katika mchezo ambao utakuwa mkali kwa vile ili Italia afuzu kucheza kombe la dunia basi mchezo huu inabidi ishinde tena ikiwezekana kwa magoli mengi ambapo katika mchezo wa kwanza Sweden ilishinda 1-0.

Ni kibarua kingine kizito kwa kocha wa Italia kwa kuisaidia timu hiyo yenye magwiji wengi kama Gianluigi Buffon ambaye ametangaza kama timu yake haitofuzu kucheza kombe la dunia basi naye atastaafu soka la timu ya taifa kama alivyofanya nyota wa Uholanzi, Arjen Robben aliyetangaza kustaafu mara baada ya kushindwa kuisaidia timu yake kucheza michuano hiyo mwakani.

Mchezo huo utaanza muda si mrefu usiku huu kwenye mishale ya saa 5 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.