Klabu ya Rayo Valecano B ambayo ni zao la klabu ya Rayo Valecano ya nchini Hispania imetoa kali ya mwaka ambayo huwezi tegemea kuiona popote haswa kwenye soka la sasa la ushindani.
Ilikuwa hivi, klabu hiyo ya Rayo Valecano B ilikuwa ikimenyana na Los Yebenes ambapo wakati vijana wa Rayo wakiwa wanawashambulia timu hiyo pinzani, mchezaji wao mmoja akaanguka na kumfanya mshambuliaji wa Rayo Valecano kufunga kirahisi.
Kutokana na hali hiyo kocha wa Rayo Valecano akawaambia wachezaji wake waonyeshe nidhamu ya kisoka au 'fair play' na ndipo mchezaji wa Los Yebenes akaachiwa bila kukabwa kwenda kufunga goli bila kubugudhiwa. Na matokeo ya mchezo kuwa Rayo Valecano 4-1 Los Yebenes.
Post a Comment
Post a Comment