Klabu ya Simba Sc leo imeuteka jiji la Mbeya mara baada ya kupata ushindi muhimu wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons ya mkoani Mbeya.
Simba imepata ushindi huo wa kwanza dhidi ya timu hiyo ambayo imekuwa ikiipa tabu sana klabu ya Simba iendapo mkoani huko.
Goli hilo la muhimu likifungwa dakika ya 84 ambapo mfungaji alikuwa ni John Bocco, usajili mpya aliyesajiliwa katika dirisha kubwa la usajili akitokea Azam Fc.
Ushindi huo unaifanya Simba kutimiza alama 22 na kuzidi kujiweka kileleni.
Matokeo ya michezo mingine;
Majimaji 2-1 Mbao
Stand united 0-0 Mwadui
Ruvu Shooting 1-0 Ndanda
Post a Comment
Post a Comment