Ilikuwa ni mchezo unaosubiriwa sana, kati ya wababe wa jiji la London, kaskazini mwa London.
Arsene Wenger amefanikiwa kumgaragaza Mauricio Pochettino na Tottenham yake kwa magoli 2-0 huku magoli ya Arsenal yakifungwa na Mustafi na Alexis Sanchez.
Kwa ushindi huo unaifanya Arsenal kufikisha alama 25 sawa na Chelsea yenye alama 25 ila Arsenal akizidiwa kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa.
Pochettino anaendelea na mfululizo wa kiwango kibovu dhidi ya timu sita za juu ambapo kati ya timu hizo ameshapoteza michezo dhidi ya Chelsea aliofungwa 2-1, dhidi ya Man utd aliofungwa 1-0 na leo amekubali kichapo ugenini cha mabao 2-0.
Je tunaweza kuita ni kuporomoka kwa Tottenham? Ikiwa na michezo 12 imevuna alama 25 tu.
Post a Comment
Post a Comment