Huu ndio utamu wa soka, ligi kuu Uingereza imetimua vumbi tena leo ambapo timu kubwa zimefanya vizuri kasoro Tottenham aliyechezea kichapo mbele ya Arsenal katika uwanja wa Fly Emirates kwa kunyukwa magoli 2-0.
Morata ang'aa tena
Baada ya mchezo uliopita ambapo Morata aliifungia goli la pekee Chelsea katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Man utd na leo tena ameifungia tena Chelsea katika ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya West Bromwich huku Morata akifunga goli moja.
Magoli mengine yakifungwa na winga, Eden Hazard aliyefunga mara mbili na Marcos Alonso akimaliza.
Chelsea baada ya ushindi huo imefanikiwa kupanda kutoka nafasi  ya nne mpaka nafasi ya tatu ikimshusha Tottenham aliyefungwa na Arsenal mapema siku ya leo.
Man city yazidi kung'aa
Ni ngumu kueleweka ni lini atapoteza mchezo, ambapo mpaka sasa katika michezo 12 aliyoingoza Man city, kocha Pep Guardiola hajapoteza mchezo hata mmoja na kusuluhu mmoja tu. Akiiongoza tena leo klabu hiyo kuitandika Leicester magoli 2-0.
Magoli ya Man city yakifungwa na Gabriel Jesus na Kevin De Bruyne.
Salah ang'aa tena;
Jina la Mohammed Salah huenda likawa linaimbwa zaidi kwa sasa pale kwa mashabiki wa Liverpool pale ambapo nyota huyo ni kama amekuja kuuteka ufalme wa Sadio Mane pamoja na Phillip Coutinho mara baada ya Salah kuonekana anaibeba sana klabu hiyo mara baada tena leo kuifungia Liverpool magoli mawili huku akiiongoza kushinda 3-0.
Salah ambaaye anagombania tunzo ya BBC kama mchezaji bora kutoka Afrika alianza kwa kufunga kwa goli zuri kwa mtindo wa 'kuzungusha' akifunga akiwa nje ya eneo la hatari kabla ya kuongeza tena kwa kufunga kwa uwezo wa kipekee. Kabla ya Coutinho kuja kuongeza goli la tatu na kufanya mchezo kuisha Klopp akiifunga kwa mara ya kwa klabu ya Southampton magoli 3-0.
POGBA & LUKAKU WAITEKA MAN UTD
Kati ya vitu ambavyo vinazungumzwa kwa sasa pale jijini Manchester huenda vikawa ni vitu viwili, ni nani wa kumzuia Man city? lakini pia ubora wa Pogba na Lukaku.
Hii inatokea mara baada ya klabu ya Man utd kurudi katika moto wao wa kufunga magoli mengi, sio kufunga magoli mengi tu, ila kufunga magoli hayo kutokana na uwepo wa mchezaji ghali kikosini hapo, Paul Labile Pogba ambaye alikuwa nje kwa muda mrefu na ikaonekana dhahiri Man utd inapata tabu kushinda bila uwepo wake lakini inapata tabu zaidi kufunga magoli mengi.
Hii imetokea mara baada ya Man utd kuwagaragaza vijana wa Newcastle kwa magoli 4-1. Na huku Lukaku akifuta ukame wa magoli kwa kutofunga katika michezo 7 iliyopita.
Wafungaji wa Man utd wakiwa ni Smalling, Martial, Lukaku na Pogba.
Matokeo mengine;
Afc Bournemouth 4-0 Huddersfield
Burnley 2-0 Swansea
Crystal Palace 2-2 Everton
Arsenal 2-0 Tottenham

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.