Mchezaji kiungo wa klabu ya Barcelona, Jose Paulinho ameeleza sababu iliyomfanya ajiunge na klabu hiyo katika kipindi cha dirisha kubwa lililopita akitokea Guangzhou Evergrande ya nchini China.

Paulinho aliyesajiliwa na Barca kwa dau la paundi milioni 35 amesema Messi na Neymar ndio waliomshawishi yeye atue klabuni hapo.

"Neymar alishawai kunambia kwamba nijiunge na Barca kwa vile nitakuwa mwenye furaha nikiwa hapa" alieleza Paulinho akimwelezea Neymar ambaye kabla alikuwa mchezaji nyota klabuni hapo kabla ya kuachana nayo na kujiunga na PSG.

"kuna mchezo Brazil tulicheza na Argentina, ndipo akaja (Messi) na kunambia angependa kama ningejiunga na Barcelona, nami nikamwambia kwa kuwa ye kataka hivyo basi nitajiunga na Barca" aliongeza Paulinho akimwelezea Messi jinsi alivyomshawishi ajiunge na klabu hiyo.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.