Ukisema chanini, wenzako wanasema watakipata lini.
Hicho ndicho kinachoonekana kwa Michael Emenalo ambaye alikuwa mmoja wa viongozi wa klabu ya Chelsea akishuhurika na maendeleo ya klabu haswa katika usajili.
Michael Emenalo sasa ni kama anawaambia mashabiki wengi wa Chelsea ambao walikuwa wakimchukia wakiamini yeye ndiye anaifanya Chelsea ifanye usajili mbovu ingawa toka alipoajiriwa na klabu hiyo mwaka 2011 akiisaidia klabu hiyo kutwaa mataji mengi yakiwemo ligi kuu mara tatu, kombe la Ueropa na klabu bingwa ya Ulaya.
Sasa Emenalo amepata ajira kama aliyoiacha Chelsea ambapo sasa amesainishwa mkataba na wakurugenzi wa klabu ya AS Monaco ambako huko anatakiwa kuanza kazi muda wowote kuanzia sasa.
Emenalo aliandika ujumbe wa kuachana na kazi katika klabu ya Chelsea ambapo hakueleza sababu rasmi ya kuachana na kazi hiyo ambayo mpaka sasa haijapata mtu wa kuishika huku Frank Lampard akitajwa kuiwania.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.