Kuelekea katika droo ya kupanga makundi ya kombe la dunia mwaka 2018 siku ya ijumaa hii tarehe 1 ambapo upangwaji wa makundi hayo kutamaanisha ufunguzi rasmi wa michuano ya kombe la dunia itakayofanyika nchini Urusi ambapo droo hiyo itapangwa jijini Moscow nchini humo.
Kocha wa Argentina, Jorge Sampaoli ametaja timu ambayo hataki akutane nayo iwe kwenye makundi au hata kwenye hatua za mbele kama timu hizo zikifuzu.
"Ujerumani. Sitamani kukutana nao maana ni mabingwa kwenye kujilinda" alisema Sampaoli, kocha wa zamani wa klabu ya Sevilla.
Ujerumani ndiyo timu ambayo Sampaoli anapiga maombi ili asikutane nao.
Alipoulizwa pia kufanya kazi na mchezaji mkubwa duniani kama Lionel Messi, kocha Sampaoli alisema "ni bahati kwangu kuwa hapa, ni bahati kwangu kufanya kazi na mchezaji mkubwa duniani kama Lionel Messi." alisema Sampaoli.
Post a Comment
Post a Comment