Sayansi na teknolojia ni moja ya nyanja inayokuwa kila iitwapo leo. Watu wanapata ujuzi na umaarufu na hata kumudu maisha na hata kutajirika kutokana na kukua kwa sayansi na teknolojia.

Smartphone ni moja kati ya zao la sayansi na teknolojia, ni chombo cha mawasiliano lakini kinachoifanya dunia kuwa kama kijiji. Aliyeko Tanzania leo kwa muda huu akiwa na smartphone anaweza akapata habari iliyotokea muda huu nchi yoyote iliyo mbali na Africa.

Kampuni ya Lenovo ni moja kati ya kampuni kadhaa zilizojikita kutengeneza vifaa mbalimbali vya kisayansi na teknolojia. Hivi karibuni kampuni hiyo ilitangaza kutoa bidhaa mpya ya smartphone ambayo uwezo wake ni tofauti kidogo na bidhaa nyengine za smartphone. Inachoifanya kuwa tofauti na bidhaa nyengine ni kwamba yenyewe inaweza kupinda na kuivaa kama saa na ukaitumia kama kawaida, hii inaipa tofauti na ile bidhaa ya gear ambayo yenyewe ni saa unaivaa mkononi lakini hii siyo saa ni simu lakini inayoweza kukunjika.

Natamani siku moja nchi yangu ya Tanzania siku moja igundue kitu kitakachoitangazia dunia kwamba na sisi sio kichwa cha mwendawazimu...

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.