Kampuni ya Samsung imechelewesha uuzaji wa simu aina ya galaxy Note 7 nchini Korea Kusini , kwa sababu kampuni hiyo inahitaji muda zaidi wa kuzirudisha simu kama hizo ambazo zilikuwa na matatizo ya betri.
Kampuni hiyo ya teknolojia nchini Korea Kusini ililazimika kuzirudisha takriban simu milioni 2.4 kutokana na betri zilizokuwa zikilipuka.
Simu nyingi zilidaiwa kushika moto.
Simu hiyo ilitarajiwa kurudishwa madukani Septemba 28 lakini sasa inatarajiwa kurudi katika maduka mnamo tarehe mosi Oktoba ikiwa ndio mapema zaidi.
Mnamo Septemba 2, Samsung ilikuwa imesema itawacha kuuza simu hizo na kuomba kurudisha simu ambazo zilikuwa imeuza.
Kampuni hiyo pia iliwataka walionunua simu hizo kuwacha kuzitumia.
Post a Comment
Post a Comment