Kocha aliyetupiwa virago na chama cha soka cha nchini Italia, Giampiero Ventura huenda akawa ana furaha mara baada ya kutupiwa virago na timu hiyo mara baada ya kushindwa kuisaidia timu hiyo kufuzu kucheza kombe la dunia mwakani toka ilipowai kufanya hivyo miaka 60 iliyopita.

Kivipi Ventura atajirike wakati kafukuzwa?

Najua ni moja ya swali unalojiuliza, lakini nipo hapa kukujibu, Ventura ambaye mapema mwaka huu alisaini mkataba mpya wa kuendelea kukinoa kikosi cha Italia ambapo mkataba wake ulikuwa na thamani ya Euro milioni 1.3 na ulikuwa uishe mwaka 2020 na kutokana ametimuliwa akiwa kaitumikia timu hiyo kwa miezi nane basi Italia inabidi imlipe kile kiasi kilichobaki katika mkataba wake.

Euro 866,000 ( zaidi ya Tsh. bilioni 2) ndicho kiasi kinachotajwa kwamba Ventura anakidai chama cha soka nchini Italia.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.