Saudi Arabia imemnyonga raia wa Ethiopia aliyehukumiwa kifo baada ya kumuua mtoto, kwa mujibu wa wizara wa masuala ya ndani.
Kulingana na shirika la habari la AFP Saudi Arabia imewanyonga watu 124 mwaka huu.
Zamzam Abdullah Boric alinyongwa mjini Riyadh baada ya kupatikana na hatia ya kumnyonga msichana mdogo na kumuacha ndani ya bafu.
Raia wengi wa kigeni hufanya kazi nchini Saudia Arabia hasa kama wafanyikazi wa nyumbani.
Mara nyingi wao hulalamika kuteswa na kuwekewa uongo kuwa wametenda uhalifu katika nchi ambayo mifumo yake ya kisheria inaonekana kukosa haki.
Post a Comment
Post a Comment