Maelfu ya wenyeji wa mji mkuu wa Tanzania, Dar es Salaam wamekuwa wakipanga milolongo tangu alfajiri kuweza kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu leo Jumatatu.
Mpango huo ambao ulianza mwishoni mwa wiki uliendelea kwa siku moja zaidi kutokana na idadi kubwa ya watu waliojitokeza.
Wengi wamemuambia mwandishi wa BBC kuwa hawangeweza kukosa fursa hiyo ya kufanyiwa uchunguzi wa bure wa kimatibabu.
Swali ni je, ni kipi kitafuatia ikiwa watapatikana na matatizo ya kiafya.
Hakuna matibabu ya bure nchini Tanzania. Watu wazee wanastahili kupata matibabu ya bure, lakini sera hiyo haijatekelezwa kikamilifu.
Post a Comment
Post a Comment