Leo katika mfululizo wa ukurasa wa Wagambo 5 nakukutanisha na gwiji wa soka raia wa Brazil, Ronaldinho Gaucho ambaye kuna watu duniani kote wanaamini ndiye mchezaji bora wa muda wote.
Kama nilivyokutambulisha Wagambo 5 itahusu mambo matano ambayo mchezaji aliwai kuyapitia na kuyafanya kabla hajawa nyota.
Lakini kabla ya kuanza tutaanza kumfahamu Ronaldinho ni nani?
Jina kamili; Ronaldo de Assis Moreira
Tarehe ya kuzaliwa; 21-Machi-1980 (miaka 37)
Mahali alipozaliwa; Rio Grande de Sol, Brazil
Vilabu alivyowai kuvichezea;
Gremio (mtoto); 1987-1998
Gremio; 1998-2001
PSG; 2001-2003
Barcelona; 2003-2008
AC Milan; 2008-2011
Flamengo; 2011-2012
Atletico Mineiro; 2012-2014
Queretaro; 2014-2015
Fluminense; 2015
Tarehe ya kuzaliwa; 21-Machi-1980 (miaka 37)
Mahali alipozaliwa; Rio Grande de Sol, Brazil
Vilabu alivyowai kuvichezea;
Gremio (mtoto); 1987-1998
Gremio; 1998-2001
PSG; 2001-2003
Barcelona; 2003-2008
AC Milan; 2008-2011
Flamengo; 2011-2012
Atletico Mineiro; 2012-2014
Queretaro; 2014-2015
Fluminense; 2015
Sasa tuingie katika wagambo (kabla hajafanikiwa) kabla hajawa mwanajeshi (nyota)
Mgambo 1; Ronaldinho alizaliwa katika familia ya mwanasoka, baba yake mzee Joao de Assis Moreira alikuwa ni mwanasoka wa klabu ya mtaani ya Esporte Clube Cruzeiro huku pia akiwa mfanyakazi wakati mama wa Gaucho alikuwa ni muuguzi hospitalini akiitwa jina la Dona Miguelina Eloi Assis dos Santos.
Mgambo 2; Meneja wake ni kaka yake akiitwa jina la Roberto ambaye yeye alishakuwa mchezaji wa klabu ya Gremio kabla ya kuwekwa nje kutokana na majeraha wakati dada yake na Ronaldinho, akiitwa Deisi ndiye anahusika na uandaaji wa mikutano ya waandishi wa habari ambapo Ronaldinho akiwa muhusika.
Mgambo 3; Ronaldinho alianza kufahamika kutokana na ufundi wake wa kuchezea mpira aliouanza akiwa na miaka 8 na kucheza katika michezo ya mtindo huru (football freestyle) kabla ya jina lake kuvuma zaidi mara baada ya kufunga magoli 23 peke yake katika ushindi wa 23-0, magoli yote akifunga mwenyewe katika mchezo wa soka mtaani.
Mgambo 4; Mwaka 2007 akiwa mwanasoka wa klabu ya Barcelona alishawai kupewa uraia wa Hispania licha ya kuwa mbrazili.
Mgambo 5; Ronaldinho ndiye mchezaji wa pili na wa mwisho kuwai kushangiliwa na mashabiki wa Real Madrid katika uwanja wa Santiago Bernabeu akiwa anaichezea Barcelona mara baada ya kufunga magoli mawili na kuonyesha kiwango bora. Mchezaji wa kwanza kufanyiwa hivyo alikuwa ni Diego Maradona mwaka 1983.
Dongo; Ronaldinho wakati anakua alikuwa anavutiwa na nyota kama Diego Maradona, Romario, Ronaldo de Lima na Rivaldo
Post a Comment
Post a Comment