Ulikuwa ni usiku mtamu, usiku wenye furaha kubwa haswa kwa mashabiki wa Liverpool mara baada ya kushuhudia timu yao ikifuzu kwa kishindo mara baada ya kumsabanga Spartak Moscow magoli 7-0.
Alikuwa nyota wa kibrazili, Phillipe Coutinho ndie aliyefanya maajabu kwa kutupia magoli matatu peke yake, huku Sadio Mane akifunga mara mbili na Salah akafunga mara moja na jengine kufungwa na Firmino.
Kwa matokeo hayo yanaifanya Liverpool kufikisha alama 12 akiwa kileleni mwa kundi lake akifuatiwa na Sevilla ambao wote hao wamefuzu kucheza hatua ya 16 bora.
Matokeo mechi za Uefa:
Maribor 1-1 Sevilla
Real Madrid 3-2 Borrusia Dortmund
Tottenham 3-0 Apoel
Feyenoord 2-1 Napoli
Shakter donetsk 2-1 Manchester city
RB Leipzig 1-2 Besiktas
FC Porto 5-2 AS Monaco
Post a Comment
Post a Comment