Hapa ndipo utamu wa soka unapokuja, utamu wa soka sio uwanjani tu, hata nje ya uwanja kuna utamu wake. Kocha wa klabu ya Shakter Donetsk, Paulo Fonseca amehuzuria katika mkutano na waandishi wa habari hapo jana akiwa amevaa kama shujaa na mwigizaji wa filamu Zorro.
Kocha huyo ameamua kuvaa hivyo mmara baada ya kufanikiwa kuisaidia klabu yake kufuzu kucheza hatua ya 16 bora katika ligi ya mabingwa Ulaya baada ya kuifunga Manchester city.
Kocha huyo amevaa vazi hilo ambapo aliwai kuahidi kuwa atavaa hivyo endapo tu atafanikiwa kufuzu kucheza hatua hiyo lakini pia kama ataifunga Manchester city. Na alifanikiwa kuwafunga 2-1 lakini pia akafanikiwa kuipeleka Shakter katika hatua ya 16 bora.
Post a Comment
Post a Comment