Ulikuwa ni usiku mwengine wenye radha halisi ya soka la kibingwa, mara baada ya viwanja zaidi ya vitano vikijaza mashabiki katika michuano ya klabu bingwa Ulaya.
Mengi yametokea usiku wa leo, lakini haya ni baadhi yake;
Man utd kufuzu kwa kishindo
Klabu ya Manchester united ilihitaji alama moja tu kuweza kufuzu kucheza hatua ya 16 bora ambapo ilikuwa na kibarua cha kutafuta hiyo alama moja dhidi ya klabu ya nchini Urusi, CSKA Moscow ambapo mchezo huo ulichezwa katika uwanja wa Old Trafford.
Man utd wakianza kufungwa mapema na nyota wa CSKA, Dragovic kabla ya Romelu Lukaku kuchomoa na Marcus Rashford kufunga jengine na kuwapatia alama tatu, baada ya kushinda 2-1.
Chelsea yamaliza wapili
Hawakuwa saaana na shida ya kupambana sana, kwa vile walishafuzu tayari, ila walichokihitaji ni kushinda mchezo huu ili imalize nafasi ya kwanza katika kundi C, ila kwa sare aliyoipata ya 1-1 dhidi ya Atletico Madrid na ushindi wa AS Roma akimfunga Qarabag 1-0 inamaanisha Chelsea imemaliza nafasi ya pili huku AS Roma akiwa kileleni. Lakini pia Atletico Madrid ikienda moja kwa moja Europa League.
Bayern Munich yarudisha makali
Mara baada ya kufanya vibaya kwa timu hiyo pindi ikiwa chini ya kocha Carlo Ancellotti, sasa makali ya Bayern yamerudi mara baada ya kumbabatiza PSG kwa mabao 3-1, magoli ya Bayern yakifungwa na Tolliso aliyefunga mara mbili na Roberto Lewandowski akifunga jengine wakati kwa upande wa PSG, goli lao likifungwa na Kylian Mbappe.
Matokeo mechi nyengine UEFA;
Olympiacos 0-1 Juventus
Barcelona 3-1 Sporting CP
Benfica 0-2 Basel
Celtic 0-1 Anderlecht
AS Roma 1-0 Qarabag

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.