Aliyewai kuwa kocha wa wababe wa Bayern Munich, Carlo Ancellotti ambaye alitimuliwa mwezi oktoba baada ya kupata kipigo kutoka kwa PSG na mwenendo mbovu wa klabu yake leo ametoa neno juu ya sababu iliyomfanya kutimuliwa klabuni hapo.
"kama klabu haitokuwa pamoja na wewe kama kocha, basi huwezi kufanya kitu." alisema Ancellotti akimaanisha kuondoka kwake Bayern ni baada ya bodi ya klabu hiyo kumtenga na kutompa heshima kabisa.
"unakuta unamweka nje mchezaji, akienda kuonana na viongozi wa bodi wale viongozi wanakuwa pamoja naye na wanakutenga wewe kama kocha" aliongeza Ancellotti alipokuwa anafanya mahojiano na chombo kimoja cha habari nchini Italia.
Lakini Ancellotti alipoulizwa kuhusu kocha wa sasa Jupp Heynckes ambaye ameirudisha Bayern Munich kwenye ubora wake na hata kuirudisha kileleni mwa msimamo wa ligi kuu, mwenyewe Carlo alisema "kajitahidi kuiweka timu kwenye hali nzuri, karudisha nidhamu na hali ya ushindi. Nampongeza kwa hilo"
Vyombo kadhaa vya habari vilikuwa vikisema kwamba kuondoka kwa Carlo Ancellotti klabuni Bayern ni kutokana na mahusiano mabovu ya kocha huyo na nyota wa klabu hiyo.
Post a Comment
Post a Comment