Kuelekea mchezo wa vigogo wawili, Manchester united itakapomkaribisha Manchester city utakuwa ni mchezo mgumu ambao kila mtu anausubiri, kwanza kutokana na ubora wa timu hizo kwa sasa ambapo Manchester city inaongoza katika msimamo ikifuatiwa na Manchester united inayoshika nafasi ya pili katika msimamo huo.
Lakini pia utanogeshwa na makocha wa timu hizo ambapo kila mmoja ni bora kwake huku wakiwa na mfululizo wa mataji, Jose Mourinho na Pep Guardiola wa Manchester city.
Kuelekea katika mchezo huo, Pep Guardiola amesema "Muhimu ni kupambana na kushinda, sio kupata kiburi kisa rekodi. Rekodi ipo na inaweza kuvunjwa ila ushindi katika mchezo huo ni muhimu"
Guardiola anaifukuzia rekodi ya Arsenal ya kushinda michezo 14 ambapo mpaka sasa kashinda 13 na kuongoza kwa alama 08 tofauti na Man utd inayoshika nafasi ya pili.
Na kama Guardiola akishinda mchezo huo unaochezwa jumapili, atakuwa kaizidi Man utd kwa alama 11 na kama Man utd itashinda itapunguza pengo la alama 8 mpaka alama 5 zitakazomfanya aikaribie zaidi.
Post a Comment
Post a Comment