Mwisho wa wiki hii kutakuwa na mchezo wa watani wa jadi yaani Manchester city ikimenyana na Manchester united ambao wote wanatokea jiji la Manchester.
Mchezo huo utanogeshwa kutokana na nafasi za timu hiyo zilivyo katika msimamo wa ligi kuu Uingereza ambapo Man city anaongoza huku Man utd akifata, huku akiwa kaachwa kwa alama nane.
Sasa kulikuwa na wasiwasi kwamba huenda kocha wa Manchester city angeukosa mchezo huo.
Kwanini Pep angefungiwa?
Kulikuwa na wasiwasi kwa kocha Pep Guardiola kuukosa mchezo huo kutokana na mashtaka yanayomkabili ambapo alikuwa akichunguzwa na chama cha soka cha nchini Uingereza, FA mara baada ya kuongea na mchezaji wa timu pinzani wakati mchezo ukiwa unaendelea dhidi ya Southampton.
Ambapo kwa mashtaka hayo yangeweza kumfanya Guardiola afungiwe mechi kadhaa ambapo huenda angeukosa mchezo huo muhimu dhidi ya watani wa jadi.
Lakini chama hicho kimetengua mashtaka hayo na kuthibitishwa kuwa kocha huyo hatofungiwa michezo yoyote.
Post a Comment
Post a Comment