Timu ya taifa ya Kilimanjaro ambayo inawakilisha Tanzania Bara imepoteza tena mchezo wake muhimu katika michuano ya Cecafa Chalenji yanayofanyika nchini Kenya.
Tanzania Bara imepoteza mchezo huo kwa mabao 2-1 dhidi ya Rwanda magoli ya Rwanda yakifungwa na Nshuti na Abeddy huku goli la Tanzania Bara likifungwa na Lyanga.
Kwa matokeo hayo yanaifanya Tanzania Bara kushika mkia katika kundi lake ambapo kuna timu za Libya, Rwanda, Zanzibar pamoja na Kenya.
Post a Comment
Post a Comment