Uongozi wa timu za taifa za Afrika Kusini maarufu kama Bafana Bafana na uongozi wa Burkina Faso umepanga kwenda katika mahakama ya kimichezo ili kupinga ushindi wa timu ya Senegal iliyoupata wiki iliyopita katika mchezo dhidi ya Bafana Bafana ambapo Senegal ilishinda 2-0 na kufanikiwa kufuzu kucheza kombe la dunia.
Afrika Kusini inadai matokeo ya kwanza ya timu hiyo dhidi ya Senegal ambapo Afrika Kusini ilishinda 2-1 katika mchezo uliochezwa mwezi Novemba mwaka 2016 na baadae kufutwa na FIFA mara baada ya kugundulika mwamuzi aliochezesha mchezo kua aliwai kufungiwa kujihusisha na mchezo wa soka, na ndipo mchezo huo kurudiwa na Senegal kushinda 2-0.
Na sasa Bafana Bafana inataka matokeo yaliyofutwa ndio yatumike au laah mchezo huo urudiwe tena, ambapo kwa upande wa Burkina Faso inabidi amfunge Cape Verde kwa magoli mengi ili afuzu katika kundi lenye timu za Senegal, Bafana Bafana, Burkina Faso na Cape Verde.
Senegal leo inashuka uwanjani dhidi ya Bafana Bafana kukamilisha mchezo wa mwisho na huku Burkina Faso akimenyana na Cape Verde.
Kama Mahakama ya michezo ikikubali rufaa hiyo basi Bafana Bafana atakuwa na alama 7 akishika nafasi ya 3 huku Burkina akiwa na alama 6 na Senegal alama 8 akishika msukani.
Na ili Burkina Faso afaidike na hukumu au rufaa ya matokeo ya kwanza kutumika itabidi amfunge Cape Verde magoli mengi na huku Senegal na Bafana Bafana zitoke sare.
Msimamo wa Kufuzu kombe la Dunia 2018 kwa Afrika; Kundi

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.