Mwafrika Francis Kone, 26 ambaye ni raia wa Togo akiwa na asili ya Senegal ameshinda tunzo ya FIFA ya kuonyesha mpira wa kiungwana (fair play) huku akiwapiku nyota kama Gianluigi Buffon na Cristiano Ronaldo.
Kone ameshinda tunzo hiyo ya FIFA mara baada ya klabu yake ya nchini Jamhuri ya Czech, Slovacko FC ilipomenyana na klabu ya Bohemians, na katika shambulizi moja ambalo klabu ya Bohemians, mlinda mlango wake aligongana na beki wake na kudondoka chini na kupata tatizo ambalo bila ya Francis Kone huenda kipa huyo angepoteza maisha palepale.
Baada ya kudondoka kipa yule akapata tatizo na kujikuta akianza kumeza ulimi wake kabla ya Kone kuona hilo na kwenda na kumpa huduma ya kwanza kwa kumuingizia kidole mdomoni na kuzuia kipa huyo asimeze ulimi, huduma ambayo inaelezwa kama isingefanyika kwa haraka basi kipa huyo, Martin Berkovec angepoteza maisha.
Baada ya tukio hilo, FIFA wakampatia tunzo ya 'fair play' nyota huyo ambaye inaelezwa alishawai kuwaokoa maisha watu wanne kwa huduma kama hiyo.
"Ni jambo la heshima kwangu na sikutarajia kupata zawadi hii. Lakini napenda kuwaambia mchezo wa mpira ni mchezo wa kiraafiki (fair play) na ili kuwaziilishia kwamba ni mchezo wa kirafiki licha ya mara nyingi kunitukana kwa kuniita nyani lakini sikujali na nimewaokoa" alisema Francis Kone ambaye anadai huwa anakutana na ubaguzi wa rangi nchini humo kutokana na rangi yake.
Post a Comment
Post a Comment