Mchezaji nyota wa Argentina, Paulo Dybala ametuma ujumbe mzito kwa wakongwe wa timu ya taifa ya Italia ambao jana walipoteza mchezo uliomaanisha hawatocheza kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi.
Kupitia mtandao wa Instagram, nyota huyo aliandika "Nilikuwa pamoja na nyinyi usiku wa jana, na niliumia pamoja nanyi, ningependa sana kukutana nanyi #Urusi katika kombe la dunia langu kwa mara ya kwanza, nyinyi ni wababe na tunaweza kushinda pamoja..salamu kwenu" ambapo ujumbe huo aliwatumia wachezaji wenzake anaocheza nao timu moja, Giorgio Chiellini, Barzagli na Gianluigi Buffon.
Post a Comment
Post a Comment