Huenda ukawa sio msimu mzuri kwa nyota wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo juu ya kiwango anachokionyesha uwanjani lakini kwa upande wa familia jamaa anajijenga, na ni kama ubora wake wa kufunga uwanjani ameuleta kwenye ngazi ya kujenga familia.

Jioni ya leo, nyota huyo ameshuhudia akipata mtoto mwengine na mchumba wake Georgina Rodriguez ambaye amejifungua kwenye hospitali moja mjini Pozuelo.

Aliana Martina ndilo jina la mtoto huyo.

Na kama ulishuhudia mchezo wa juzi wa timu yake ya taifa, Cristiano hakuwepo ata kwenye orodha ya wachezaji wa akiba ambapo timu yake ya taifa ilimpa ruhusa ya kwenda kumshuhudia mtoto wake.

Aliana ni mtoto wa nne kwa nyota huyo ambaye miezi saba nyuma, alishuhudia pia watoto wake wakizaliwa ambao walikuwa mapacha. Kwa hivyo sasa Cristiano Ronaldo ana watoto wanne.

Hongera sana Cristiano Ronaldo

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.