Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Rwanda na aliyekuwa kocha msaidizi wa Rayon Sports FC ya nchini humo, Ndikumana amefariki dunia.

Hamad Ndikumana Katauti ambaye anajulikana vyema kama mme wa mwigizaji wa Tanzania, Irene Uwoya amefariki huku chanzo kikitajwa kuwa ni ugonjwa wa moyo.

Ndikumana amefariki akiwa na miaka 39 huku akiitumikia klabu ya Rayon Sports kama kocha msaidizi, kwa mujibu wa afisa habari wa klabu hiyo, Gakwaya Oliver anadai "Ndikumana kabla ya mauti kumkuta alikuwa akilalamika kwamba kifua kinamuuma na kuomba apewe soda ya baridi baada ya kupewa alianguka na kupoteza maisha" lakini bado wanafatilia chanzo cha kitabibu kuelewa ni kipi kimesababisha umauti huo.

Pole kwa ndugu na jamaa wa Ndikumana aliyewai kuitumikia klabu ya Stand United ya Tanzania akiwa kama mchezaji.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.