Ni wiki nyengine tamu, wiki nyengine ya utamu wa soka, wiki nyengine baada ya mfululizo wa mechi za kimataifa, sasa tunarudi kwenye wiki ya utamu.
Utamu mmojawapo wiki hii, unaanzia kule kwenye jiji la Madrid ambapo wababe wa jiji hilo yaani Real Madrid na Atletico Madrid zitamenyana.
Lakini utamu huu utanogeshwa pale ndugu wawili watakapokutana, Theo Hernandez anayeichezea Real Madrid na ndugu yake Lucas Hernandez anayeichezea Atletico.
Kuelekea katika mchezo huo, mama mzazi wa ndugu hao, For Py Laurence ametoa neno kuhusu mchezo huo na jinsi anavyojisikia kwa watoto wake kukutana.
"Ni jambo zuri kwangu, kuwaona watoto wangu wakiwa kwenye klabu kubwa Hispania na hata duniani" alisema mama huyo aliyewalea watoto hao akiwa kama mama bila kuwa na baba.
"nilikuwa nawapeleka kila siku mazoezini, nilikuwa nawapa moyo na kuwashauri kila siku, sio kuhusu maisha tu ila hata mpira"
"hawajapata nafasi ya kudumu katika vikosi vya kwanza lakini huwa nawahamasisha na kuwapa moyo kwamba inabidi wapambane kufikia malengo" aliongea mama huyo huku akisema katika mchezo huo atafurahi kuwaona lakini pia atakuwa shabiki wa timu zote.
Jambo la kushangaza juu ya ndugu hawa wawili ni kwamba wote wanatumia mguu wa kushoto kama mguu wenye nguvu kwao.
Post a Comment
Post a Comment