Jioni ya leo ligi kuu ya Tanzania bara itatimua vumbi tena katika baadhi ya viwanja. Lakini mechi au mchezo unaovuta hisia za wapenzi wengi wa kandanda katika ligi hii ni mchezo kati ya Yanga African ya Dar es salaam watakapokipiga na watoto wa kimakonde kutokea mkoa wa Mtwara, Ndanda FC.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezeka katika uwanja wa Uhuru ambao watu wengi wamekuwa wakiuita "shamba la bibi". Mchezo huo utachezeka saa 10 Alasiri ambapo timu zote zinahitaji points tatu ili kujiweka kwenye nafasi nzuri huku Yanga wakitaka ushindi baada ya mchezo uliopita kusuluhu na African Lyon kwa goli 1-1, ambapo pia Ngamia hao wa jangwani wakiongozwa na kocha wao mpya, Lwandamina aliyefanya mabadiliko kadhaa kwenye benchi la ufundi na katika kikosi chake cha kwanza. Wakati Ndanda akipoteza michezo yake miwili ya mwisho kabla ya huu wa leo.

Post a Comment
Post a Comment