Usiku wa leo kutakuwa na mchezo wenye mvuto sana pale Uingereza katika dimba la St.Mary's park ambapo wenyeji wa uwanja huo Southampton watawakaribisha vijana wa Maurio Pochettinho, Tottenham Hotspur ambao mwenendo wao umekuwa sio mzuri kwa sasa.
Ikumbukwe moja kati ya vionjo vya mechi hii ni pale Victor Wanjama kijana wa Kikenya atakaporudi kwa mara ya kwanza katika kiwanja ambacho msimu uliopita alicheza akiwa kama mwenyeji akiwa na jezi za Southampton wakati usiku wa leo atarudi akiwa kama mgeni katika uwanja huo akiwa katika jezi za vijana wa London kaskazini, Tottenham.
Huu ni mchezo muhimu kwa kila mtu ambapo Southampton wanaoshika nafasi ya 8 katika ligi wakiwa na points 24 watahitaji kushinda na kupanda mpaka nafasi ya 7 ambayo inashikiliwa na Everton wenye points 26. Wakati Tottenham wao watahitaji kushinda ili kujiweka sawa maana mpaka sasa wanalingana points na Manchester united wote wakiwa na points 33 lakini Totts wapo nafasi hiyo kwa kuwa na faida ya magoli ya kufungwa na kushinda.

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://pbs.twimg.com/media/DMZ1UrCXcAAa6Ij.jpg} Johnny malcom is the proffesional public health officer,graphic designer and amature mechanical engineer who likes blogging as much as eating. {facebook#https://www.facebook.com/Runc2} {twitter#https://twitter.com/Runcxx} {google#https://plus.google.com/u/0/113916418534820565109} {pinterest#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {youtube#YOUR_SOCIAL_PROFILE_URL} {instagram#https://www.instagram.com/official.seeker/?hl=en}
Powered by Blogger.