Romelu Lukaku, mshambuliaji wa Ubelgiji ambaye anaitumikia klabu ya Manchester united jana ameweka rekodi katika timu yake ya taifa.
Lukaku amekuwa mfungaji bora wa muda wote katika timu yake ya taifa mara baada ya kuifungia goli moja katika mchezo wa kirafiki walipocheza dhidi ya Japan.
Mchezo huo uliisha kwa Ubelgiji kushinda 1-0, goli lililofungwa na Lukaku na kumfanya kufikia rekodi hiyo akitimiza magoli 31 akiwa na miaka 24 tu.
Post a Comment
Post a Comment