Kocha wa timu ya taifa ya Hispania, Julen Lopetegui ametoa sifa kedekede kiungo mshambuliaji wa timu hiyo anayeichezea klabu ya Real Madrid, Isco.
Kocha huyo alipohojiwa mara baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Costa Rica ambapo mchezo uliisha kwa Hispania kuondoka wa mabao 5-0 wafungaji wakiwa Jordi Alba, Alvaro Morata, David Silva aliyefunga mara mbili na Iniesta akimalizia la mwisho. Kocha huyo alisema "Isco ni mmoja kati ya wachezaji bora duniani, sikutegemea aliyoyafanya na nategemea vingi kutoka kwake.
Isco alicheza vizuri katika kipindi cha kwanza ingawa kipindi cha pili alitoka kwa majeruhi.
Isco ambaye ndiye mchezaji mwenye magoli mengi kwa sasa pale klabuni Real Madrid akiwa kaifungia timu hiyo magoli 4 na kutengeneza mengine matatu katika michezo 11 anaonekana kuwa tegemezi zaidi klabuni hapo huku akimwacha Cristiano Ronaldo.
"kuhusu majeruhi yake, Isco alipata majeruhi toka katika mchezo wa klabu yake dhidi ya Girona ingawa hayakuwa makubwa. Na hata jana ni kama alitoneshwa kwa hivyo taarifa zaidi kuhusu majeruhi yake tutatoa majibu kesho (leo jumapili)" alisema kocha wake.
Post a Comment
Post a Comment