Shirika la utangazaji nchini Uingereza, BBC limetoa orodha ya wachezaji wanaowania tunzo ya mchezaji bora kutoka Afrika.
Wanaowania tunzo hiyo ni Emerick Pierre Aubameyang ambaye ni mshambuliaji wa klabu ya Borrusia Dortmund ya Ujerumani na timu ya taifa ya Gabon, Sadio Mane ambaye ni winga wa klabu ya Liverpool inayoshiriki ligi kuu Uingereza na timu ya taifa ya Senegal, Mohammed Salah ambaye amesajiliwa na klabu ya Liverpool akitokea As Roma ya nchini Italia na timu ya taifa ya Misri, Victor Moses ambaye ni mchezaji wa klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya Nigeria na wa mwisho ni Naby Keita ambaye yeye aliisaidia klabu ya RB Leipzig ya nchini Ujerumani kung'aa huku kwa timu yake ya taifa ikiwa ni Guinea.
Je ni nani kushinda tunzo hiyo?
Post a Comment
Post a Comment